"NIPE SIKUACHI" YA HUSSEIN MACHOZI KUACHIWA WIKI CHACHE ZIJAZO

BAADA ya kukaa kimya kwa miezi mingi bila ya kutoa wimbo, Hussein Machozi anatarajia kuachia kibao kipya wiki chache zijazo.

Kibao hicho kinajulikana kwa jina la “Nipe Sikuachi” ambao umetayarishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa bongofleva, Man Water wa Studio za Combination Sound.

“Combination yangu ya mimi na Water sidhani kama kuna kitu cha mchezo hapo,” alisema Machozi ambaye amethibitisha kuanza kufanya kazi rasmi kwa uangalizi wa lebo ya mtayarishaji huyo mashuhuri Bongo.


Machozi alisema kuwa video ya kibao hicho imefanyika nchini Italia, Gressoney Italy na kwamba kuna mabadiliko makubwa ukilinganisha na mandhari ya video zilizozoeleka kila siku.

No comments