OMMY DIMPOZ KUPAKUA NNE KWA MPIGO… asema zitakuwa funga kazi ya mwaka 2017

OMMY Dimpoz anatarajia kufyatua nyimbo nne, huku mbili kati ya hizo akiwa ameshirikisha baadhi ya wasanii na nyingine kuimba mwenyewe, ambazo zitakuwa ni za “funga kazi” mwaka huu.

Alisema, atashirikisha wasanii wenzake kwa kuwa anatambua kwamba kolabo ni jambo la kawaida katika muziki na anaweza kushirikisha msanii kutoka lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz.

Alisema kuwa haoni tatizo kufanya kolabo na masanii wa lebo hiyo kwa madai kwamba muziki ni biashara na pia anaangalia muunganiko wa sauti yake na msanii anayemshirikisha.


Dimpoz amekuwa akitamba na wimbo wake wa “Kajiandae” ambao ameimba kwa kumshirikisha nyota mwenzake, Ali Kiba.

No comments