OZIL AIWEKEA IMANI ARSENAL KUMALIZA LIGI KATIKA NAFASI NZURI MSIMU HUU

WINGA wa timu ya taifa ya Uingereza na Arsenal, Mesut Ozil amesema kwamba pamoja na kuanza vibaya Ligi msimu huu lakini anaamini klabu hiyo itamaliza ikiwa na mafanikio makubwa.

“Tumeanza vibaya ndio, lakini hiyo ni changamoto kwetu wachezaji na kocha wetu. Ninaamini tutamaliza Ligi tukiwa katika nafasi nzuri ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.”

“Naamini kwamba kikosi hiki kinaweza kufanya makubwa zaidi ya yale ambayo yamewahi kufanyika huko nyuma. Ni kikosi imara sana,” amesema.

“Lakini unaona kwamba kila wakati tumekuwa tukiporomoka na kuyumba. Mimi nadhani sasa tuko vizuri zaidi ya huko nyuma na yatupasa kuwa na imani hiyo,” amesema.

Ozil ambaye amekuwa akikosa baadhi ya mechi kutokana na majeruhi, amesema kuwa kikosi chao kiko vizuri na akampongeza Sanchez na kumfananisha na greda linaloweza kupasua mahali popote.


“Namuona kama greda linalojenga barabara. Lakini namtazama Sanchez kama mtu ambaye amefungwa betri yenye nguvu wakati wote. Hii inanipa raha sana,” amesema.

No comments