OZIL ASEMA ANALAUMIWA BILA MSINGI WOWOTE KWA ARSENAL KUYUMBA

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil anaamini analaumiwa bila msingi wowote kutokana na matatizo yanayoikumba klabu hiyo.

Ozil, 28, alilaumiwa tena baada ya Arsenal kupokea kichapo cha 5-1 ugenini kwa Bayern Munich katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya usiku wa Jumatano.

Lakini wakala wake amesema kwamba mchezaji huyo hapaswi kulaumiwa kwani matatizo ya Arsenal ni mfumo mzima.

“Ukosoaji ni kawaida mchezaji anapocheza vibaya,” wakala huyo Dkt Erkut Sogut aliiambia BBC Sport na kuongeza:
“Lakini Mesut anahisi kwamba watu hawaangalii vyema uchezaji wake na badala yake analaumiwa bure baada ya timu kupata matokeo mabaya.”

Ozil alijiunga na Arsenal kutoka Real Madrid mwaka 2013 kwa ada ya pauni mil 42.4 iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya England.

Alitua Emirates akiwa na sifa ya kuwa mmoja wa viungo wa kati wazuri sana duniani lakini uchezaji wake karibuni umekosolewa sana.


Dhidi ya Bayern, alikamilisha pasi 20 pekee ambazo ni sawa na alizokamilisha kipa wa Bayern Manuel Never.

No comments