Habari

PEP GUARDIOLA ASAKA SAINI YA LUKASZ PISZCZEK MAN CITY

on

BOSI wa Manchester City, Pep
Guardiola ameonyesha nia ya kumsainisha beki wa kati, Lukasz Piszczek.
Lukasz Piszczek ni kati ya
wachezaji muhimu kwa sasa walio katika kiwango cha juu, ana kipaji cha kuweza
kucheza katika klabu yoyote kubwa, hivyo City haipaswi kumwacha.
“Ana sifa moja kubwa nayo ni
kuwakabili washambuliaji wa timu pinzani na anajua kujipanga hasa katika
mazingira magumu.”
“Kizuri ambacho ni sifa yake ya
ziada ni kwamba ni mzuri katika kupanga safu ya ulinzi, hivyo ni mtu muhimu kwa
sasa katika kiwango cha soka la dunia,” alizungumza Pep Guardiola na kunukuliwa
na The Goal.
“Sikuwahi kumshawishi kwa kiasi
kikubwa lakini natambua vyema uwezo alionao ambao ni muhimu kwetu kama klabu
kufanya jitihada kumpata na kuimarisha safu ya ulinzi.”

“Kama atafanikiwa kutua kwetu
nitajisikia furaha kupitiliza kwasababu ndoto ya fikra zangu itakuwa imetimia.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *