PEP GUARDIOLA APANIA MABAO ZAIDI MAN CITY LIGI YA MABINGWA ULAYA

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa timu yake inaweza kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iwapo hawatafunga katika mechi ya marudiano hatua ya 16 bora dhidi ya Monaco.

Katika mchezo wao wa kwanza, Man City walitoka nyuma mara mbili na hatimae wakafanikiwa kuwalaza viongozi hao wa Ligi ya Ufaransa mabao 5-3, mechi ya kusisimua iliyochezwa uwanja wa Etihad.

Mechi ya marudiano itachezwa Machi 15.
“Tutasafiri Monaco na kufunga mabao mengi kadri iwezekanavyo,” Guardiola alisema baadae.

“Hilo ndilo lengo langu. Ni vigumu kusonga tusipofunga bao.”

Monaco waliongoza 2-1 na 3-2 kabla ya City hawajajikwamua na kupata ushindi.

Mechi hiyo inaongoza kwa kufungwa mabao mengi miongoni mwa mechi za mkondo wa kwanza hatua ya muondoano katika miaka 25 ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Guardiola anatarajia mechi iwe wazi sana klabu hizo zitakapokutana tena.


Anahisi hiyo ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na mashambulio makali ya Monaco ambao wamefunga mabao 76 katika mechi 26 za Ligi.

No comments