PEP GUARDIOLA APIGA HESABU ZA KUMNG'OA DANI ALVES JUVENTUS

KAMA ukisikia uchokozi ndio huu. Klabu ya Manchester City imesema inafikiria kumsajili beki wa kulia wa Juventus ambaye aling’ara sana katika klabu ya FC Barcelona, Dani Alves.

Habari zinasema kwamba kocha wa sasa wa Manchester City, Pep Guardiola anaona kwamba kuna haja ya kumsajili beki huyo ambaye alikuwa akimtumia vyema wakati akikinoa kikosi cha Barcelona.

Gazeti la Daily Stars limeandika kwamba hata Dani Alves mwenyewe anapenda kufanya kazi na kocha wake huyo wa zamani na hivyo anaonyesha kwamba maisha yake kwenye kikosi cha Juventus ni mafupi zaidi.

Nyota huyo raia wa Brazil amekuwa akicheza kwa mafanikio makubwa katika nafasi ya mlinzi wa kulia na kocha wa Manchester City amesema kwamba hana wasiwasi Dani ni mmoja wa mabeki bora hapa duniani.

“Kwangu mimi huyu ndie beki bora wa kulia kwa sasa. Najua kuna watu wanaona kama nafasi yake ni ngumu kwasababu ameshaondoka katika klabu ya Barcelona, lakini sioni kama kuna beki wa kumzidi kwa sasa,” amesema Guardiola.


Pep Guardiola amesema kwamba bado na mahusiano mazuri na Alves kiasi kwamba akiwa kocha, anataka kuimarisha timu yake kwa kuwa na watu anaowafahamu kwamba wanapigania ushindi.

No comments