PHILIPPE COUNTINHO ASEMA LIVERPOOL INA NAFASI YA UBINGWA

NYOTA wa klabu ya Liverpool raia wa Brazil Philippe Countinho ameitabiria makubwa timu yake hiyo kwa kuamini kuwa ina nafasi ya kubwa ya kupambana kwa ajili ya ubingwa wa premier msimu huu.

Alipoulizwa kwanini ana imani hiyo, Countinho mwenye umri wa miaka 23 alijibu kuwa anajivunia ubora wa kocha na kwamba ana mbinu kubwa za kufundisha soka la kisasa.

“Ukiniuliza mimi kwanini ninaamini tuna nafasi ya ubingwa ninaweza kukwambia jambo moja kuwa Klopp ni kocha bora kwasababu ameibadili timu yangu pale alipopewa jukumu.”

“Liverpool ya sasa ni tofauti na ile iliyokuwa chini Brendan Rodgers, kuna tofauti kubwa hata ya namna timu inavyocheza kwa wachezaji kushirikiana dimbani.”

“Tangu atue Anfied ameonyesha mambo mapya ambayo sisi kama wachezaji tunaweza tukawa sehemu ya kuzungumzia mabadiliko haya,” alisisitiza mwanandinga huyo raia wa Brazil.

“Tunacheza tukiwa na furaha na imani kubwa chini ya Klopp, kama atapewa muda zaidi wa kuendelea kuwa hapa nina imani kuwa kila jambo linaweza kubadilika na hata timu kurejea katika kiwango cha soka la zamani.


“Tupo katika mwendo wa mafanikio tunarudi katika mstari wetu wa siku nyingi nyuma ambapo soka letu lilikuwa kiwango chetu cha kawaida."

No comments