Habari

PICHA 14: SUPER KAMANYOLA YA MWANZA ILIVYOKULA ‘VALENTINE’ VILLA PARK

on

Bendi bora ya dansi kwa ukanda wa kanda ya ziwa Victoria, Super
Kamanyola Band ya Mwanza, katikati ya wiki hii ilimimina uhondo mkubwa
iliyoaacha simulizi kwa wakazi wa jiji hilo.
Super Kamanyola ilijikita katika ukumbi wao wa nyumbani, Villa Park
siku ya Jumanne na Jumatano ikiwa ni wiki maalum ya kuadhimisha Siku ya
Wapendanao Duniani (Vallentine’s Day).
Bendi hiyo yenye wakongwe kama Beno Villa, Parashi na Omar Seseme,
ikatesa na nyimbo mchanganyiko – za kwao na zile za kunakili kutoka kila pembe
ya dunia.

Pata picha 14 za onyesho la Super Kamanyola la siku ya Jumatano ndani
ya Villa Park.
 Benno Villa akipapasa kinanda na kuimba
 Zuhura dansa wa Super Kamanyola
 Kisura mmoja wa madansa wa Super Kamanyola
 Dispatch mwimbaji wa zamani wa Mashujaa na FM Academia naye yupo Super Kamanyola
 Kamodee akikunguta bass gitaa
Allan mkali wa magitaa yote
 Mwimbaji mkongwe Parashi akifanya vitu vyake
 Difenda Rapa wa Super Kamanyola 
 Omar Seseme kwenye mpini wa solo
Mashaka kwenye drums
 Dansa wa zamani wa Mashujaa Band, Super Nywamwela Jr akiitumikia Super Kamanyola
 Waimbaji na madansa wa Suiper Kamanyola wakishambulia jukwaa
Fundi mitambo Fadhili akiwe kwenye eneo lake la kujidai

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *