PICHA 15: ISHA MASHAUZI ALIVYOISIMAMISHA KAHAMA …apiga nyomi la kufa mtu


Jumnne usiku Isha Mashauzi aliufanya mji wa Kahama usimame kwa burani moja tu ndani ya ukumbi wa Kikwetu Kwetu.

Ilikuwa ni kama vile Kahama hakukuwa na burudani katika viwanja vingine vya starehe kwa namna watu walivyofurika kwa wingi kwenye show yake ya Valentine’s Day.

Licha ya ukumbi huo wa Kikwetu Kwetu kuwa nje kidogo ya mji, lakini mashabiki wa muziki walijitokeza kwa wingi kiasi kwamba hata pa kuweka mguu ilikuwa shida.

Isha akapiga show ya ‘jeshi la mtu mmoja’ kwa kusimama jukwaani kuanzia saa 6.30 hadi 9 usiku na kuwapeleka msobe msobe wakazi wa Kahama.

Nyimbo kama “Nani Kama Mama”, “Tugawane Ustaarabu”, Nimpe Nani”, “Jiamini”  “Mamaa Mashauzi” na “Sura Surambi” zilikuwa ni baadhi ya nyimbo zilizoiteka show.

Pata picha 15 za onyesho hilo la Isha Mashauzi.
 Isha Mashauzi akiwajibika jukwaani
 Ni wakati wa kutupia masauti matamu
 Makamuzi yanaendelea
 Kila mtu na pozi lake!
 Isha mbele ya umati wa mashabiki wake
 Mdau wa muziki Hassan Kipoi (kulia) akifuatila show sambamba na 'jirani' yake
 Isha Mashauzi
 Isha akikusanya kijiji
 Umati uliofurika ukumbini
 Palikuwa hapatoshi
 Isha akiimba "Nimpe Nani"
 Raha zikiendelea kumiminika
 'Stage' ilikuwa si ya kitoto
 Watangazaji wa Kahama FM Dj Rammy (kushoto) na Rama TZ wakifuatilia onyesho la Isha
Isha Mashauzi akiwa na DJ wa ukumbi wa Kikwetu Kwetu

No comments