Habari

PICHA 16: JAHAZI MODERN TAARAB ILIVYOFANIKISHA TUKIO LA KUADHIMISHA MIAKA 10 YA BENDI YAO

on

USIKU wa Jumamosi Jahazi Modern Taarab walifanya sherehe ya kishindo ya miaka 10
ya bendi yao na zifuatazo ni picha 16 za namna matukio yalivyoendelea ndani ya
kiwanja cha Darlive, Mbagala, Dar es Salaam ilipofanyikia shoo hiyo.

 Kiongozi wa Jukwaa wa Jahazi Modern, Ally Jay akipapasa kinanda kwa mbwembwe huku baadhi ya mashabiki wakiwa wamemzunguuka
 Mmoja wa ma MC wa tukio hilo, Aisha Mbegu kutoka Times Fm akisherehesha kwa raha zake
 Hapa Aisha Mbegu akiwa na MC mwenzake, Dk. Kumbuka katika kutia “amsha amsha” kwa mashabiki
 Ally Jay akiwa kazini
 “Bosi Kichefuchefu” Prince Amigo akiimba kwa mashamsham wimbo “Tba ya Mapenzi”
 Dk. Kumbuka akiendelea kunogesha kwa porojo za hapa na pale
 Mcharazaji gitaa la Solo, Hemedi Emelaa akicharaza nyuzi kwa umakini mkubwa
Mkurugenzi Hamis Boha akikata keki kufanikisha tendo la kufikisha miaka 10 ya bendi yao
 Moja ya keki zilizokatwa na kuliwa kwenye tukio hilo la miaka 10 ya Jahazi Modern Taarab
 Mdau maarufu wa muziki, Juma Mbizo akilishwa keki 
Mwimbaji Mish Mohammed nae akilishwa keki
Hivi ndivyo ukumbi wa Darlive ulivyokuwa umetapika 
 Mmoja wa wasanii waliowahi kupitia Jahazi Modern, Twaha Malovee akiimba kwa hisia
 Safu ya waimbaji wa Jahazi Modern wakilishambulia jukwaa
Mkung’utaji gitaa la besi, shomary Zizou akifanya yake jukwaani

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *