Habari

PICHA 35: MAKAMUZI YA USIKU WA ISHA MASHAUZI TEMA MATE CHINI, MANGO GARDEN YAZIZIMA … Isha afanya vitu adimu

on

Usiku wa Isha Mashauzi uliofanyika jana usiku ndani ya Mango Garden,
ulibamba ile mbaya.
Isha akisindikizwa na bendi yake ya Mashauzi Classic, akadhiirisha
uwezo wake wa kusimama jukwaani kwa muda mrefu kwa kuimba nyimbo tisa kali.
Lilikuwa ni onyesho lilipambwa na shangwe kibao, ikiwa ni sehemu ya
sherehe za kuzaliwa kwa Isha Mashauzi ambapo keki na shampen zilifurika kwa
wingi kutoka kwa mashabiki wake mbali mbali.
Isha akiwa ametinga jeans nyeusi na tshirt nyekundu aliimba nyimbo
mbili “Kila Mtu na Mtuwe” na “Nani Kama Mama” kabla ya kupisha shughuli za
tafrija ya kuzaliwa kwake.
Awamu ya pili Isha akarejea jukwaani katika mwonekano mpya, safari hii
akiwa ametinga gauni la njano, hatua iliyozua makeke ya furaha kutoka kwa watu
waliofurika Mango Garden.
Katika awamu hiyo ya pili, Isha alikamua nyimbo saba mfululizo “Sura
Surambi”, “Kismet”, “Nimpe Nani”, “Mapenzi Hayana Dhamana”,  “Acheni Kuniambana”, “Tugawane Ustaarabu” na
“Thamani ya Mama”.
Mbali na show ya Mashauzi Classic, pia kulikuwa na burudani ya Kibao
Kata pamoja na segere kutoka kwa Siza Mzongele.

Pata picha 35 za onyesho hilo la Usiku wa Isha Mashauzi lililoutapisha
ukumbi wa Mango Garden.
 Hashim Said akiimba “Bonge la Bwana”
 Kali Kitimoto kwenye kinanda
 Asia Mzinga akiimba “Ubaya Haulipizwi”
Abdumalick Shaaban akiimba “Kupendwa Bahati Yangu”
 Shaaban wa Kumwaga (kushoto) na Mkude wakionyesha ufundi wao wa kucheza na magitaa
Shabiki wa Isha Judith Marcus kwenye red carpet
 Mambo ya Kibao Kata
 Kibao Kata hiyo
 Mzee Mbizo akiteta na mamaa Maureen 
Team Mashauzi Family
 Rahma Amani akiimbo moja ya nyimbo za Mashauzi Classic
 Isha Mashauzi akihojiwa katika red carpert 
 Isha Mashauzi alivyoonekana katika awamu yake ya kwanza jukwaani
 Isha Mashauzi akifanya yake
 Tafrija ikiendelea
Isha Mashauzi akifungua shampen
 Baadhi ya keki zilizofurika ukumbini
 Isha Mashauzi (kulia) akikata keki
Isha na meneja wake Sumaragar
 Siza akisema machache kuhusu Isha Mashauzi
 Siza Mazongele akiburudisha
 Siza akifungua moja ya shampen
Mtangazaji wa Radio Uhuru MC Jojoo naye alikuwepo
 Saida Ramadhan akiimba “Pendo la Ukakasi”
 Mango Garden ilifurika vizuri mno
 Mashabiki wakimkodolea macho Isha Mashauzi
 Awamu ya pili Isha alitokelezea namna hii
 Isha Mashauzi jukwaani
 Isha na shabiki wake wa kuitwa Mamuu Original
 Isha Mashauzi akikamua mbele ya mashabiki wake
 Ilikuwa full shangwe
Taswira ya Mango Garden jana usiku

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *