PICHA 7: WATU NA NYOTA ZAO! ISHA MASHAUZI ALIVYOKATISHA SHUGHULI ZA WAKAZI WA KAHAMA MCHANA KWEUPEEEE


Wiki chache zilizopita Isha Mashauzi alikuwa gumzo kwenye mitaa ya mji wa Kahama, pale wakazi wa mji huo walipoacha shughuli zao na kujazana sehemu alipokuwa.

Wakati Isha akiwa mtaani kwenye moja ya salon za mji huo kujiandaa na show yake Valentine’s Day (iliyofanyika usiku katika ukumbi wa Kikwetu kwetu), wakazi wa mji huo wakatonyana juu ya uwepo wa mwimbaji huyo katika eneo fulani.

Taratibu kijiji kikaanza kukusanyika na pindi mwimbaji huyo alipotoka nje, akakutana na umati mkubwa wa mashabiki wake.

Isha hakuwa na hiyana, alipoteza dakika kadhaa kusalimiana na mashabiki wake kabla ya kuingia kwenye gari la wenyeji wake na kuondoka. Ilikuwa ni hatua iliyowasisimua watu wengi.
 Watu na nyota zao asikwambie mtu
 Isha Mashauzi akiagana na mashabiki wake
 Mashabiki wa Isha huko Kahama
 Isha akiongea neno flani kwa mashabiki wake kabla ya kuondoka
 Namna ya Isha kuondoka eneo hilo ilikuwa shida
Mashabiki ni kama vile walikuwa hawataki aondokeNo comments