POLISI MAREKANI WAANZA KUCHUNGUZA TUKIO LA WIZI NYUMBANI KWA NICKI MINAJ

JESHI la polisi kwenye jimbo la Los Angeles, Marekani linachunguza wizi uliofanyika kwenye nyumba ya msanii Nicki Minaj wiki iliyopita.

Msanii huyo wa muziki wa Hiphop na R&B amekombwa mali zenye thamani ya dola za Kimarekani 175,000.

Polisi wamesema kwamba wizi huo ulitokea kwenye nyumba ya kifahari ya Minaj iliyopo eneo la Beverly Hills lakini mwanamuziki huyo hakuwa nyumbani wakati wa tukio.

Wamefafanua kwamba nyumba hiyo ilivunjwa wakati wa uvamizi huo na baadhi ya nguo za nicki Minaj kuibiwa.


Baada ya kukosa fedha taslim, wezi hao walimalizia hasira zao kwa kuharibu fenicha mbalimbali vikiwemo picha na chupa za manukato viliyokuwa ndani. 

No comments