PORTO WAITEGA ATLETICO MADRID KUHUSU KUMNASA NICOLAS GAITAN

KLABU ya Porto ya Ureno imetega Atletico Madrid na sasa imerejea azma yake ya kutaka kupata saini ya Nicolas Gaitan.

Taarifa za ndani za klabu hiyo ya nchini Ureno zinasema kuwa uongozi umetoa ridhaa kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo kwa gharama ambayo haikutajwa.

Mpango wa mwaka huu ni kama wanakumbusha kidonda cha mwaka jana ambapo klabu hizo mbili ziliingia vitani kwa kila mmoja kuhitaji mchezaji wa upande wa pili.

Katika harakati hizo, Porto walikuwa wanamwania Nicolas Gaitan katika usajili wa majira ya kiangazi lakini sasa wameamua kufanya kweli.


Wakisikiliza tetesi hizo, Porto wameweka mezani dau la pauni mil 29 kwa ajili ya kiungo huyo.

No comments