PSG YAZIVAA MAN UNITED, ATLETICO VITA YA KUMWANIA MLINZI WA VILLAREAL

KLABU ya Paris Saint-Germain inapigana vikumbo na baadhi ya klabu zinazomfukuzia mlinzi wa Villareal, Adrian Gomez ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo katika timu ya CD Leganes inayoshiriki La Liga nchini Hispania.

Gomez amekuwa akihusishwa na kujiunga na PSG katika usajili ujao wa dirisha la kiangazi lakini Liverpool inalazimika kuweka dau la ziada mezani la pauni mil 24 kwa ajili ya jembe hilo.

Pamoja na hilo, majogoo hao wa jiji inawabidi kupambana kwa ajili ya beki huyo kisiki kwani anawaniwa kwa karibu na Manchester United.

United wametajwa katika dili la kumfukuzia kiungo huyo wa Atletico Madrid kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha mashetani wekundu hao.

Lakini taarifa zinasema kuwa PSG wameshamaliza mazungumzo ya awali na Gomez kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kinachopambana kwa ajili ya ubingwa wa msimu huu.


Awali Liverpool waliweka mezani dau la pauni mil 15 kwa ajili ya mchezaji huyo kabla ya Atletico hawajaweka bayana kuwa dau la mchezaji huyo ni mil 23.

No comments