QUEEN LATIFAH KUIRUDIA UPYA FILAMU YA “LIVING SINGLE” YA MWAKA 1990

RAPA mahiri wa kike na mwigizaji anayetisha, Queen Latifah amesema anaitoa upya filamu yake iliyotikisa miaka ya 1990, iitwayo “Living Single”.

Mwigizaji huyo kutoka Chicago, mwenye miaka 46, amefichua hayo juzi katika kipindi kimoja cha Tv akiwa na waigizaji Kim Coles na Kim Fields.


“Kwa leo siwezi kusema sana ila naweka wazi kuwa nairudia filamu yangu ya “Living Single”, kuna sababu nyingi za kufanya hivyo ila kubwa ni ujumbe wake,” alisema Queen Latifah.

No comments