RAFAEL NADAL WA TENISI KUJIFUA KABLA YA MICHUANO YA WIMBLEDON

MCHEZA tenisi, Rafael Nadal anatarajia kupasha kabla ya kushiriki mashindano ya Wimbledon.

Nadal atacheza katika mashindano ya mabingwa wa Aegon yatakayofanyika Juni, mwaka huu.

Bingwa huyo wa mataji 14, ataungana na mwingereza Andy Murray katika michuano hiyo ambayo Nadal aliwahi kuwa bingwa mwaka 2008.

“Watu walioandaa mashindano hayo wako vizuri. Kwangu itakuwa njia sahihi ya kujiandaa na mikiki mikiki ya Wembledon,” alisema mcheza tenisi huyo.

Mkurugenzi wa mashindano, Stephen Farrow alisema: “Nadal ni miongoni mwa wachezaji tenisi wakubwa kwa kipindi kirefu, amekuwa maarufu kuchezea klabu ya Queen.”

Mapema mwezi huu Nadal alisema angeshiriki michuano ya mabingwa wa Aegon katika kipindi chote cha maisha yake ya tenisi.

Tayari BBC imetangaza kuripoti mashindano hayo mpaka mwaka 2024.


Michuano hiyo itaanza Juni 19 mpaka 24, mwaka huu. 

No comments