RAPHAEL VARANE WA REAL MADRID ANUKIA BAYERN MUNICH

TAARIFA za tetesi za usajili wa mwishoni mwa juma lililopita zinamtaja nyota wa Real Madrid, Raphael Varane kuwa ana asilimia kubwa ya kutua Bundesliga ambako anawaniwa na mabingwa watetezi, Bayern Munich.

Daily Star imemueleza Varane kama ni mchezaji wa awali aliye katika malengo ya klabu hiyo inayosaka tena taji la ubingwa wa Ujerumani.

Hata hivyo, Bayern wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vigogo wengine wa soka barani Ulaya wakiwemo Liverpool, Juventus na Paris Saint-Germain ambao wamo katika mbio za kuwania saini ya Rafael Varane.

Varane amekuwa akikosa namba ya kudumu katika kikosi cha Los Brancos cha msimu huu baada ya kocha wa Real Madrid, Zenadine Zidane kuwapa nafasi kubwa walinzi Sergio Ramos na Pepe.

Varane mwenye umri wa miaka 23 ameelezwa kutoficha mapenzi aliyonayo kwa kocha Jose Mourinho tangu akiinoa Chelsea hata alivyokuwa ndani ya Real Madrid.


Mourinho alikuwa akimwamini Varane kiasi cha kupagawa mara kwa mara tofauti na sasa ambapo amekuwa akipangwa kwa nadra na zidane.

No comments