RAY C AANZA KUTESTI ZARI LA MUZIKI UPYA KWA KUACHIA KIBAO “UPEPO”

MSANII wa kike wa Bongofleva aliyepata kutikisa kutokana na uwezo wake wa kunengua, Rehema Chalamila “Ray C” baada ya kupitia kipindi kigumu sasa anataka kujaribu tena.

Ray C hajatoa kazi yoyote tangu aanze kupambana na vita ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya na hivi sasa ameibuka na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la “Upepo”.


Msanii huyo bali na uwezo mkubwa wa kunengua, pia aliweza kutunga nyimbo zenye kuliwaza, ambazo zilikolezwa utamu na sauti yake mororo iliyowapagawisha mashabiki wa Bongofleva.

No comments