RAYVANNY ASEMA: “IKO SIKU TU NITAPIGA KOLABO NA ALI KIBA”

MSANII anayekuja kwa kasi katika muziki wa Kizazi Kipya kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rayvanny, mesema kuwa hawezi kumfungia vioo Ali Kiba kwa vile tu hapatani na Diamond Platnumz anayemiliki lebo anayotoka yeye.

“Ninajua kwamba Kiba ni mpinzani mkubwa wa bosi wangu Diamond Platnumz lakini mimi sina tatizo na Kiba na ikitokea nafasi ya kufanya nae kolabo nitafanya kwa sababu muziki ni biashara,” alisem,a Rayvanny.

Msanii huyo alisema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha radio jijini Dar es Salaam na kuweka wazi kila anapokutana na Kiba amekuwa akisalimiana naye na kupiga stori.

“Kiba huwa ananisifia kuwa ninafanya kazi nzuri hivyo ikitokea siku ninaweza kufanya nae kolabo kwani cha kutambua ni kwamba wote tunafanya muziki ambao ni biashara na mashabiki wetu wanatamani kusikia kazi zenye muunganiko wa wasanii tofauti,” alisema.


Kwa muda mrefu sasa wasanii hao nyota; Diamond Platnumz na Ali Kiba wamekuwa katika bifu ambalo linadaiwa linachochewa na mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii.

No comments