REFA ALIYEMPA SANCHEZ BAO LA MKONO AKUA, AWA BORA ZAIDI DUNIANI

UPO ukweli ambao hautapindishwa hata kwa moto wa tanuli kwamba Mark Clattenburg ni kati ya waamuzi bora waliobaki, si tu Uingereza bali duniani.

Anastahili kuwa mwamuzi bora kwani baada ya kuwa Pierlluig Colliina kustaafu kumekuwa na uhaba wa waamuzi na nchini Uingereza, lakini pia Howard Webb nae aliondoka Ligi Kuu na siku chache zilizopita wakati Mike Dean nae alishushwa daraja kutoka Ligi Kuu.

Mwamuzi huyu, Mark Clatteenburg amegusia kutoka moyoni mwake kabisa kwamba huenda siku moja ataondoka Uingereza.

Kutokana na utajiri wa Ligi ya China, watu wengi waliamini Clatteenburg huenda angejiunga na Ligi ya nchini humo na wengine wakisema labda refa huyo angeenda kumalizia kazi yake katika Ligi Kuu ya Marekani lakini sio hivyo.

Clatteenburg ambaye alichezesha fainali za FA na UEFA msimu uliopita, sasa anaelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kwenda kuanza kibarua kipya.

Katika taarifa iliyotolewa na chama cha waamuzi, walimtakia kila la kheri refa huyo katika majukumu mapya anayoenda kuanza katika nchi hizo za Kiarabu.

“Tunamtakia kila la kheri katika kazi yake anayoenda kuianza toka amejiunga nasi mwaka 2004 amekuwa akikua kila siku hadi kufikia kuwa kati ya waamuzi wa kiwango cha juu kabisa, Mark ameonyesha njia na kitu ambacho wengine inabidi waige utendaji wake wa kazi, amefanya makubwa sana na wote ni mashahidi wa kazi kubwa aliyoifanya msimu uliopita,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

“Mark ana kipaji cha hali ya juu na ni kati ya vitu muhimu kwa mpira wa Uingereza. Tunaamini amewahamasisha wengine wanaotamani kuwa marefa, hili ni jambo kubwa kwake na tunaamini atafanya pia vizuri huko aendako,” ilimaliza taarifa hiyo.


Clatteenburg kwa mara ya kwanza alkichezesha mpira katika Ligi Kuu mwaka 2000 akiwa na miaka 25 tu. Mechi ya mwisho ya Clatteenburg ilikuwa ni kati ya Arsenal na Hull City katika mchezo ambao aliruhusu goli la mkono la Sanchez. Clatteenburg aliwaomba radhi wachezaji wa Hull City baada ya goli hilo la Sanchez.

No comments