RONALDO AONGOZA KWA KUTENGENEZA MABAO NA KUVUNJA REKODI YA GIGGS

UNAWEZA kusema kwamba kila binaadamu amezaliwa na kipaji chake. Kuna wengine wamezaliwa kwa kuwaburudisha watu wengine.

Timu ya real Madrid ya Hispania ilikuwa uwanjani dhidi ya Napoli katika mchezo ulioisha kwa Madrid kuibuka na mabao 3-1.

Magoli ya Madrid yaliwekwa kimiani na Toni Kroos, Karim Benzema na mkata umeme wao mkubwa, Casemiro, huku Ronaldo akitoka uwanjani bila goli.

Pamoja na kuondoka bila goli usiku huo, lakini Cristiano Ronaldo alivunja rekodi iliyowekwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs.

Ronaldo ndie aliyetoa pasi iliyoleta goli la Toni Kroos na “assist” hiyo kwake ilikuwa ya 31.

Kabla ya mchezo kati ya Real Madrid na Napoli, Ryan Giggs alikuwa akishikilia rekodi ya kutoa “assist” nyingi.

Pamoja na kustaafu kucheza soka lakini bado pasi zake 30 katika mashindano ya UEFA ilikuwa ngumu kuvunjwa kabla ya mchezaji bora wa dunia kufanya hivyo dhidi ya Napoli.

Ronaldo ambaye huu ni msimu wake wa tano katika mashindano ya UEFA, anaweka rekodi yake sasa ya kuwa mchezaji mwenye pasi nyingi za mabao zaidi katika mashindano ya UEFA.


Lakini huenda Ronaldo asifurahie sana rekodi hiyo kwani ana njaa kubwa na goli akicheza dakika 523 bila kuona wavu.

No comments