SAIDA KAROLI: VIONJO VYA NYIMBO ZANGU VINA MCHANGO MKUBWA KWENYE BONGOFLEVA

NYOTA wa muziki wa asili ya kabila la Kihaya, Saida Karoli amesema kuwa vionjo vya nyimbo zake vina mchango mkubwa kwenye muziki wa Kizazi Kipya kwa madai kwamba wasanii waliovitumia wameshaonja mafanikio yake.

Vionjo vya wimbo “Maria Salome” vimetumika katika nyimbo kama “Salome” wa Diamond platnumz, “Muziki” wa Darasa na “Give It To Me” wa Belle 9 na Saida anajivunia mchango wake katika muziki huo Bongo.

“Wote hao wamechukua vionjo vya wimbo wangu wa “Maria Salome” nanyi mnajua jinsi nyimbo zao hivi sasa zinavyotamba, hivyo sina budi kujivunia kwa jinsi muziki wangu wa asili ulivyo na mchango kwenye Bongofleva,” alisema.


Alisema kuwa, nyimbo za muziki wa Kizazi Kipya za sasa zinaonekana hazidumu, yaani ni nyepesi na ndio maana baadhi ya wasanii wameamua kutumia baadhi ya vionjo vya nyimbo zake na kujikuta wakiongeza idadi ya watu wanaofuatilia nyimbo zao.

No comments