SALIF DIAO AITAKA LIVERPOOL KUMSAIDIA SADIO MANE

MCHEZAJI wa zamani na kiungo wa timu za Senegal na Liverpool, Salif Diao ameiambia timu yake ya zamani kwamba inapaswa kumsaidia Saidio Mane kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kukosa mkwaju wa adhabu ambao uliisababishia timu yake ya Senegal kuondolewa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.

Mane alivunjika moyo baada ya kukosa penati muhimu katika robo fainali dhidi ya mahasimu wao timu ya Cameroon.


Diao amesema kwamba kuna haja ya kuwa na mtazamo chanya juu ya kushindwa kwa timu ya Senegal na sio kumfanya mane kuwa ndio mchawi wao.

No comments