SERGIO AGUERO BADO YUPOYUPO SANA TU MANCHESTER CITY

MANCHESTER City haina mpango wa kumpiga bei nyota wake Sergio Aguero katika kipindi cha kiangazi.

Licha ya kuwekwa benchi katika michezo yake miwili iliyopita, klabu hiyo haifikirii kumtupia virago Aguero.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28, alisaini mkataba wa nyongeza mapema msimu huu hivyo bado ana miaka mitatu imesalia ndani ya Etihad.

Baada ya kuingizwa dakika za majeruhi katika mechi dhidi ya Swansea na Manchester City kushinda 2-1, Aguero alisema: “Nahitaji kuendelea kubaki.”

“Katika hii miezi mitatu ijayo nataka kuisaidia klabu yangu, lakini wao wataamua kama bado nina nafasi au la.”

Hata hivyo, Aguero anatarajiwa kufanya maamuzi kifikia katika kipindi cha kiangazi.

Vigogo wa klabu ya Manchester City, Jumapili iliyopita walisisitiza kwamba hawana mpango wa kuuza wachezaji.

Aguero raia wa Argentina aliingia kuchukua nafasi ya Gabriel Jesus ambaye alipata majeraha katika dakika za lala salama.


Jesus raia wa Brazil amekuwa akimweka benchi Aguero katika kikosi cha kwanza cha kocha Pep Guardiola.

No comments