SIRI YA ZLATAN IBRAHIMOVIC YAFICHULIWA KWEUPEE

WAKATI mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibraimovic amekaa kimya kuhusiana na mkataba wake licha ya kusema kuwa ametekeleza yote yanayohitajika ili mkataba wake uweze kuongezwa, kuna jambo jipya limeibuka.

Raia huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Man United msimu uliopita kwa mkataba wa mwaka mmoja na tayari amefunga magoli 20 msimu huu.

Mourinho alisema Ijumaa kuwa mshambuliaji huyo atasalia Old Trafford mwaka 2017-18 alipoulizwa kuhusu hatima yake ambapo alisema “Tutasubiri tuone.”

Wakati akijiunga na Barcelona alijiunga mkataba wa miaka mitano lakini alitumia miezi 12 tu kabla ya kuondoka.

Katika miezi hiyo 12 Kadabra alifanikiwa kuifungia Barcelona jumla ya magoli 21 katika mashindano yota hayo lakini pamoja na hayo aliamua kuondoka Barcelona ambayo kipindi hicho ilizunguukwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu akiwemo Lionel Messi na Thiery Henry.

Sasa siri ya Ibra maarufu kama Kadabra kutodumu na kutoonyesha makali yake akiwa na Barcelona imefahamika.

Inaaminika Ibrahimovic hakuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya watu katika timu ya Barcelona akiwemo Lionel Messi lakini pia uhusiano wake na kocha Pep Gurdiola nao ulikuwa chanzo cha Zlatan kuondoka.

Katika uchezaji, Messi alihitaji eneo kubwa la kucheza jambo ambalo pia Zlatan alilitaka.

Meneja masoko wa zamani wa Barcelona amefichua kwamba msuguano wa chinichini kati ya Ibra na Messi ulikuwa unamfanya afanye kile atakacho uwanja hali iliyopelekea kuondoka kwake. 

“Kwanini hakufaninikiwa Barcelona? Zlatan ni hatari na ni mashine, lakini pembeni yake kulikuwa  na mashine kadogo (Messi)."

“Naamini msuguano ule wa chini kwa chini na Messi ambao wengi hawakujua ndio uliomfanya kuamua kuondoka katika kikosi hiki,” alisema Ingla ambaye sasa anafanya kazi na timu ya Lille ya nchini Ufaransa.


Zlatani sasa yuko Uingereza huku akifunga karibu kila wiki na Messi naye akiendelea kunga’ra La Liga.

No comments