SOULJA BOY ADAI CHRIS BROWN AMEOGOPA KICHAPO NA KUJITOA KWENYE PAMBANO

MWANAMUZIKI Soulja Boy amedai kwamba Chris Brown amejiondoa kutoka kwenye pigano lao.

Wawili hao wamekuwa wakizozana kwenye mitandao ya kijamii na baadaye wakaandaa pambano la ndondi kuamua nani mkali mjini Las Vegas.

Pambano hilo lingekuwa la laundi tatu hata hivyo tarehe ya kufanyika kwa pigano hilo haikuwa imetangazwa.

Bingwa wa zamani wa ndondi duniani uzani wsa juu Mike Tyson alikuwa akimpa mafunzo Chris Brown naye Soulja Boy alikuwa akifunzwa na bingwa mwingine wa ndondi Floy Mayweather.

Lakini rapa huyo ametangaza kupitia twitter kwamba pigano hilo lililokuwa la dau la dora mil 1 halitafanyika tena.

“Meneja wa Chris Brown alimpigia meneja wangu usiku wa kuamkia leo (juzi) na kumwambia kwamba pigano halitafanyika tena na kwamba hatatia saini mkataba na nisiniulize zaidi.”

“Sitasema labda aliogopa au labla hakukuwa na sababu yoyote, nitasema tu kwamba hataki kupigana siwezi nikamlazimisha kutia saini mkataba.”

Ugomvi kati ya wawili hao ulianza baada ya Soulja Boy kupenda nakutolewa maoni picha ya Karrueche Tran mpenzi wake wa zamani wa Chris Brown kwenye Facebook.
Wawili hao walioneshana katika video wakitiana vitisho.


Mike Tyson alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba alikuwa anarekodi wimbo wa kumshambulia Soulja Boy mwezi uiliopita lakini kufikia sasa haujatolewa.

No comments