SUAREZ ALIA NA MWAMUZI “KIMEO” ALIYEMTWANGA KADI NYEKUNDU

KAMA unadhani waamuzi wanaobahatisha katika soka wako Bongo tu utakuwa unakosea sana kwani mmoja wa nyota wenye majina makubwa kabisa katika soka anasema mwamuzi aliyempa kadi nyekundu ni “kimeo”.

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez amedai kuwa ana matumaini rufani yake itakayokatwa itaweza kumwokoa asikose mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalmebaada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa fainali ya mkondo wa pili dhidi ya Atletico Madrid.

Suarez aliifungia Barcelona bao katika mchezo ambao ulishuhudia wachezaji watatu wakipewa kadi nyekundu katika sare ya bao 1-1 juzi, iliyofanya Barcelona kufuzu fainali ya nne mfululizo kwa jumla ya mabao 3-2.

Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa argentina alitolewa nje kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa Barcelona baada ya mwamuzi kudhani alimpiga kiwiko Koke katika dakika za majeruhi.

Suarez anasema kadi hiyo aliyopewa inamfanya ajisikie kucheka kwani inaonekana kama mwamuzi alidhamiria kufanya hivyo.

Suarez aliendelea kusema kuwa anataka kuona kama anaweza kukata rufani kwasababu hadhani kama alifanya kosa lolote linalostahili adhabu hiyo.


Nyota huyo amesema kwamba hana wasiwasi kuwa maamuzi ya mwamuzi wa mechi hiyo yalijaa utata na kuwa pamoja na kwamba mwamuzi ndiye mwenye hukumu ya mwisho uwanjani lakini yeye hakustahili adhabu ambayo amepewa.

No comments