SWANSEA CITY YAMNASA MSHAMBULIAJI MDOGO WAKE ANDRE AYEW

KOCHA wa Swansea City, Paul Clemente amefichua kuwa klabu yake imemnasa mshambuliaji wa Ghana, Jordan Ayew.

Ayew ambaye ni mtoto wa mwanasoka wa zamani wa Ghana, Abedi Pele, alisisimua mashabiki wa soka duniani baada ya kuifungia Ghana bao la ushindi wakati ilipoilaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 2-1 kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili.

Bao la kwanza la Ghana kwenye mchezo huo lilifungwa na kaka yake, Andre Ayew ambaye alikuwa Swansea City msimu uliopita kabla ya kuuzwa kwa pauni mil. 20.5.


Clement alisema kuwa ana matumaini Jordan ambaye wamemnunua kwa ada inayokadiriwa kuwa pauni mil 5 kutoka Aston Villa, atakisaidia kikosi hicho katika harakati za kujiokoa kutoshuka daraja Ligi Kuu England.

No comments