THEO WALCOTT AFIKISHA BAO LA 100 ARSENAL

STAA Theo Welcott amekuwa mchezaji wa 18 kufikkisha bao la 100 akiwa na Arsenal baada ya Jumatatu kutupia moja katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Suton United katika mchezo wa Kombe la FA.

Kabla ya bao hilo straika huyo wa timu ya taifa ya England alipiga Hat-trick dhidi ya klabu yake ya zamani Southampon na hivyo kumfanya afikishe mabao 99 katika mchezo mwingine wa Kombe la FA wa raundi ya nne.

Hadi sasa Welcott amefunga mabao 63 katika mechi ya Ligi Kuu, alikuwa na Arsenal 11 kombe FA na tisa katika michuano ya Ligi.


Mbali na mabao hayo staa huyo amewahi kutupia hat-trick katika mashindano yote ya soka la Uingereza na ndiye mchezaji pekee Arsenal kufunga bao katika mchezo wa fainali wa michuano ya Kombe la Ligi ya FA.

No comments