TIMU YA MCHANGANI ENGLAND YACHEKELEA KUPANGWA NA KIKOSI CHA WENGER KOMBE LA FA

TIMU ya mchangani ya Sutton United imechekelea kupangwa na vigogo Arsenal kwenye raundi ya tano ya Kombe la FA.

Sutton United inayoundwa na wachezaji wa ridhaa, itavaana na Arsenal kati ya Februari 17-20 kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa juzi Jumatatu.

Kocha wa timu hiyo, Paul Doswell amefananisha kuvaana na Arsenal sawa na mechi ya Kombe la Dunia.

“Hatuamini kwa kweli kuwa eti tumepata nafasi ya kuvaana na moja ya klabu bora barani Ulaya,” alisema Doswell.


Sutton ilikata tiketi ya kucheza raundi ya tano ya michuano hiyo baada ya kuitoa Leeds United inayoshiriki Ligi daraja la kwanza England wikiendi iliyopita.

No comments