Habari

PICHA 20: UKUMBI WA LUNCH TIME MANZESE ‘ULIVYOTAPIKA’ MIAKA MITANO YA WASHAWASHA CLASSIC MIN BAND

on

SHOO maalum
ya kutimiza miaka mitano ya bendi ya taarab ya Washawasha Classic Min Band
iliyopigwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi ndani ya Lunch Time, Manzese Tiptop, Dar es Salaam imeonekana kufana pengine kuliko
shoo zote zilizokwishapigwa hapo tangu mwaka upinduke.
Umati mkubwa
wa mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ambayo pia ilitiwa baraka na wadau na
wanamuziki mbalimbali kutoka bendi nyingine tofauti, ulidhihirisha kuwa
Washawasha ni kati ya makundi ya muziki yanayokuja juu kwa kasi hivi sasa.
Mpangilio mzuri
wa ratiba katika shoo hiyo, nao ulichangia kuchangamsha na kuifanya ionekane
bab kubwa, huku pia vibao vipya vya bendi hiyo vikiwakoleza wengi miongoni mwa
waliohudhuria ambao baadhi yao walishindwa kujizuia na kujikuta wakijimwaga
katikati kucheza.
Zifuatazo ni picha 20 za namna shoo hiyo
ilivyofanyika.  
 Aliyekuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo, Mwasiti Robert akifanya yake jukwaani
 Mcharazaji mahiri wa gitaa la Solo kutoka Yah TMK Modern Taarab, Mohammed mauji akifuatilia kwa makini shughuli hiyo
 Hii ndio keki maalum iliyoandaliwa 
 Mtangazaji Ummy Suleiman wa CITY FM (kushoto), na Mrs Maya wakishiriki zoezi la kukata keki
 Mwimbaji Dogo Amran akiwajibika jukwaani na wimbo wake mpya
 Mmoja wa wazee wa bendi, mzee Mchafu akilishwa keki
 Mwanahawa Chipolopolo akimlisha keki bosi wake, Amour Maguru
 Fadher Mauji nae akifaidi keki
 Ikafika zamu ya Mpapasa kinanda mahiri wa TOT, Juma Jerry
Hii sasa ni zamu ya Mkurugenzi wa Kongamoyo Iqujuan Ikbar 
 Kutoka kushoto ni Ashura JJ, Ummy, Father Mauji, Juma Jerry na Thabit Abdul
Bosi wa Washawasha Classic, Amour Maguru akipapasa kinanda kwa uhodari wa hali ya juu
 Mwimbaji mahiri, Omary Sosha akiburudisha mashabiki
 Mwimbaji Mwanahawa Chipolopolo akiimba baada ya kutambulishwa rasmi ndani ya bendi hiyo usiku huo
Mwimbaji mlemavu wa macho, Sofia akichetua mashabiki kwa wimbo wake mpya
 Mdau wa muziki ambaye pia ni dada wa mchezaji wa Azam FC, Sure Boy, Asha Midole nae alikuwepo
 Hapa mkali wa Kibao Kata, Kivurande Junior akipagawisha mashabiki 
 Viongozi wa bendi ya Mashauzi Classic Modern Taarab, Sumaragar Ismail (kushoto), na Makassy Ally, nao wakifuatilia kwa makini
 Mwimbaji Semeni Bhai akiimba kwa manjonjo
 Hivi ndivyo ukumbi wa Lunch Time ulivyokuwa umetapika

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *