WACHEZAJI TIMU YA TAIFA GHANA HOFU KIBAO KWA CAMEROON LEO

MSHAMBULIAJi mahiri wa Ghana “Black Star”, Jordan Ayew aliyefunga bao la kwanza katika robo fainali katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Kongo (DRC), amewaonya wenzake.

Ghana inashuka dimbani leo kuivaa Cameroon “Indomitable Lions” katika dimba la Stade de Franceville katika mechi ya nusu fainali za Kombe la mataifa Afrika.

Mchezaji huyo wa Aston Villa ya England alisema wanapaswa kuwa makini ili kumaliza ukame wa taji hilo kwa miaka 35.

“Huu ni mchezo muhimu na mgumu sana kwetu, hatutakiwi kutegemea rekodi zilizopo, Cameroon wamebadilika na walichowafanyia Senegal sote tumekiona, tunapaswa kujituma kwa nguvu zote,” alisema.


Rekodi inawabeba Ghana dhidi ya Cameroon kwani katika mechi saba walizocheza Cameroon imeshinda moja na sare tatu huku Ghana ikishinda tatu.

No comments