WACHEZAJI WA WEST HAM KUMBE WALITAKA DIMITRI ASEPE ZAKE

SASA imefichuka kwamba wachezaji wa klabu ya Westham walitaka Dimitri Payet kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuelekea Merseille.

Kulingana na mwenyekiti mwenza wa klabu hiyo, David Sullivan, wachezaji wote wa Westham walikuwa wameadhimia kwamba ni vyema nyota huyo raia wa Ufaransa akaondoka ili akili yake iwe huru, lakini pia wachezaji wengine wawe huru kiakili.

Mshambulia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 alijiunga tena na klabu yake ya zamani kwa kitita cha pauni mil 25 baada ya kudaiwa kukataa kuchezea Westham kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

“Kwa kweli hatukutaka aondoke lakini huwezi kwenda kinyume na umoja wa timu,” Sullivan alisema wakati anahojiwa na shirika la utangazaji la uingereza BBC.

Sullivan alisema kuwa Payet aliamua kutochukua mshahara wake wa Januari na hakuwa na mahusiano mema hata na wachezaji wenzake.

“Payet hakuzungumza na mtu kwa wiki sita. Amekaa kuzungumza na mtu yeyote katika timu,” alisema Sullivan.


Payet alijiunga na westham mwezi Juni, 2015 na alikuwa na mchango mkubwa katika klabu hiyo lakini imedaiwa kwamba katika siku za mwisho bamekuwa kiburi.

No comments