Habari

WAHUNI WAVAMIA FAMILIA YA SADIO MANE NA KUHARIBU GARI LENYE THAMANI KUBWA

on

JINAMIZI la Senegal kuondolewa katika mashindano
ya fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) nchini Gabon mwaka huu bado
linawasumbua raia wengi nchini humo.
Raia pamoja na mashabiki wengi wa soka waliamini kwamba
senegal inaweza kuchukua ubingwa wa AFCON.
Alikuwa ni mchezaji wao tegemeo, Sadio Mane
ambaye alikosa tuta lililowapelekea Senegal kuondolewa katika mashindano hayo.
Sasa familia ya Sadio Mane iliyoko huko Senegal
imekumbana na majanga ambayo yamesababishwa na kukosa penati kwa Mane.
Familia ya mjomba wake Mane imevamiwa na kikundi
cha wahuni ambao inasemekana walikuwa na nia ya kumdhuru mjomba wake huyo.
Mjomba wake Mane na familia yake wameripoti kuwa katika
tukio hilo vibaka waliharibu gari la mjomba yake Mane ambaye alinunuliwa na
Sadio Mane kwa kiasi cha pauni 24,000.
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kikundi
hicho kilivamia kwa hasira familia ya akina mane na kuanza kupigapiga gari hilo
lililokuwa nje ya nyumba yao huko Malika.
Wakati familia yake ikitokewa na majanga hayo,
mane yeye alikuwa katika majukumu na Liverpool.

Mane alikuwa kwenye kiwango cha juu akiiongoza
timu yake kufunga Tottenham magoli 2-0 huku kocha wake, Jurgen Klopp akimmwagia
sifa kwa kusema hakuna timu yoyote ambayo isingeathirika kumkosa Sadio Mane. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *