WAMISRI WAANZA MAJIGAMBO... wasema soka lao sasa limepanda kiwango

CHAMA cha soka cha Misri (EFA), kimesema mafanikio ya Misri kutinga fainali ya Kombe la Mataifa Afrika 
yanadhihirisha kuwa soka la nchi hiyo limepanda kiwango.

Mjumbe wa Bodi ya EFA, Hazam El-Hawary alisema, soka la nchi hiyo liliporomoka kwa kuchangiwa na vurugu za kisiasa nchini humo.

Tangu mwaka 2010 Misri ilishindwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

“Katika siku za karibuni soka la nchi yetu limeanza kurudi na hii imedhihirika kwenye mashindano haya ya mwaka huu,” alisema Hawary.


Misri leo inavaana na Burkina Farso kwenye nusu fainali ya AFCON.

No comments