WASTARA JUMA KUFUNGUA MWAKA NA FILAMU YA "HAPENDEKI"

BAADA ya kutamba na firamu iiitwayo “Karibu Dar” nyota wa Bongomuvi, Wastara Juma anatarajia kuonekana tena kwenye kazi mpya iitwayo “Hapendeki” ambayo ni ya kwanza kwake kwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa Wastara, filamu hiyo ambayo imeandaliwa na kampuni yake ya Wajey inatarajiwa kutoka Februali 13, mwaka huuu na kwamba siyo kazi ya kukosa kwani inavitu vingi vya kuburudisha na kuelimisha.

Alisema kuwa mwaka mmoja ambao amekaa bila kutoa kazi mpya umetosha kumpa nafasi ya kujipanga upya na sasa ameibukia ndani ya filamu ya “Hapendeki” ambayo ana uhakika mashabiki wa Bongomuvi watapata uhondo wa kutosha.

No comments