WEMA SEPETU ATETEA KIMYA CHAKE... awataka mashabiki kusubiri mshindo mkuu anaokuja nao

MWIGIZAJI wa bongomuvi, Wema Sepetu amesema kwamba kimya kingi kina mshindo mkuu hivyo amewataka mashabiki wake wajiandae kupata vitu vikali kutoka kwake katika mwaka huu 2017.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Wema aliandika katika posti yake ya kwanza kwa mwaka huu katika mtandao wa kijamii akitoa ahadi hiyo kuwa kuna mambo mazuri kutoka kwake ndani ya mwaka huu.

“Mwaka uliopita niliahidi kwamba mwaka huu 2017 utakuwa ni mwaka wangu wa kazi nyingi na naendelea kusisitiza kuwa kuna mambo mengi mazuri yanakuja,” alisema wema.


Nyota huyo aliyefuatiliwa na watu zaidi ya mil 2.5 alifuta kila kitu katika akaunti yake ya Instagram na kuacha hivyo kwa miezi kadhaa na kuzua maswali kuhusu alikojichimbia.

No comments