WIZ KHALIFA ALETEWA TAARIFA YA KIFO CHA DADA YAKE KATIKATI YA BIRTHDAY YA MWANAE

RAPA mahiri Wiz Khalifa aliarifiwa kifo cha dada yake, Dorien Thomaz “Lala” Jumatatu wiki hii akiwa katikati ya sherehe.

Rapa huyo alikuwa katika pati ya kukata na shoka na marafiki zake pamoja na mtalaka wake, Amber Rose alipopata taarifa za kifo cha dada yake Lala.


Mkali huyo wa kibao “Black And Yellow”, alisema baadae kuwa alikuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa kwa mwanae, Sebastian aliyetimiza miaka mine.

No comments