Habari

YAH TMK KUTAMBULISHA MPYA EQUATOR GRILL VALENTINE DAY

on

YAH TMK
Modern Taarab wanatarajiwa kuitumia shoo ya Valentine watakayotumbuiza pamoja
na African Stars ‘Twanga Pepeta’ ndani ya Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally,
Dar es Salaam, kutambulisha nyimbo zao mpya.

Omary Teggo
ambaye ni mmoja wa mabosi ndani ya Yah TMK amesema kuwa, anaamini shoo hiyo
itakuwa na msisimko wa hali ya juu kutokana na namna walivyojipanga kukonga nyoyo
za mashabiki wao wa Wilaya ya Temeke.
Amesema kuwa, wanazo nyimbo kadhaa mpya ambazo hazijawahi kutua masikioni mwa mashabiki wao na kwamba kwa mara ya kwanza kabisa nyimbo hizo zitarindimishwa ndani ya Equator Grill siku hiyo ya Valentine Day watakakopiga na Twanga Pepeta. 
“Nawaomba mashabiki wetu wote wa maeneo ya Mtoni pamoja na wilaya nzima ya Temeke kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kufaidi uhondo huo wa nyimbo zetu mpya tuliowaandalia,” amesema Teggo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *