ZFA YATAKIWA KUBADILIKA NA KUBORESHA LIGI KUU… yasisitizwa kuachana na soka la mazoea

KUTOKANA na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kuahidi kujenga uwanja wa kisasa wa soka, viongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), wametakiwa kubadilika.

Wito huo umetolewa na mmoja wa wanasoka walioitangaza vyema Zanzibar kabla ya kugeukia ukocha, Seif Bausi anayeinoa Zimamoto.

Alisema, ili uwanja huo uweze kuleta manufaa katika soka la Zanzibar, ni lazima ZFA wahakikishe wanabadilika na kuboresha Ligi Kuu ya kisiwa hicho na Ligi Daraja la Kwanza.

Alifafanua kuwa mfumo wa Ligi ya Zanzibar haujawa wa kukuza soka bali ni wa mazoea, jambo ambalo amedai halina tija kwa soka la sasa.

“Ahadi ya serikali kujenga uwanja wa kisasa itakuwa na manufaa kama ZFA nao watabadilika na kuamua kukuza soka kwa vitendo,” alisema.


Ahadi ya uwanja wa kisasa ilitolewa na rais Ally Mohammed Shein wakati wa kufunga mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Januari 13, mwaka huu.

No comments