ZINEDINE ZIDANE AMFUNGULIA MILANGO JAMES RODRIGUEZ

WAKATI ambapo James Rodriguez anahusishwa na tetesi za kutaka kutua kwa mashetani wekundu wa jijila Manchester, klabu yake ya Real Madrid inathibitisha kuwa milango iko wazi kwa timu inayomuhitaji ifanye michakato ya mapema.

Rodriguez mwenye umri wa miaka 26 amekuwa na mafanikio makubwa tangu atue mwaka 2014 katika kikosi cha Los Brancos.

Akinukuliwa juu ya suala la kuondoka kwa mwanandinga huyo, kocha Zinedine Zidane alisema: “James ni mchezaji ambaye kwa sasa anaweza kuondoka Real Madrid.”

“Tetesi za sasa ni za kweli kwani Real Madrid haina mpango wa kumbakiza kikosini straika huyu.”

"Tunatambua luwa Manchester United na Chelsea wamo mbioni kutaka saini yake, nadhani ni muda mwafaka kwao kufanya kwa ajili ya kumsajili.”


Wakati James akivumishwa kujiunga na moja ya timu za Premier, kuna taarifa za mwanandinga huyo kutaka kwenda kusakata soka katika Ligi ya nchini China ambako kunadaiwa kuna klabu zenye utajiri unaofanya wachezaji kulipwa kiwango kikubwa cha mishahara.

No comments