ADHABU YA MECHI TATU KWA IBRAHIMOVIC YAANZIA MECHI YA MAN UNITED DHDI YA CHELSEA


Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic ambaye amefungiwa kwa mechi tatu, ataanza kuitumikia adhabu hiyo katika mchezo wa FA Cup dhidi ya Chelsea Machi 13.

Ibrahimovic amekumbana na adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko  Tyrone Mings wa Bournemotuh kwenye mchezo wa Premier League Jumamosi iliyopita.

Mechi zingine atakazokosa Ibrahimovic  ni kati ya Middlesbrough Machi 19 na West Brom April moja. Michezo yote hiyo miwili ni ya Premier League.

Ibrahimovic amekubali adhabu lakini Mings  ambaye naye alikabiliwa na adhabu kama hiyo kwa kumsigina kichwani Ibrahimovic amesema atakata rufaa, hatua ambayo mwisho wa siku inaweza ikamrefushia adhabu iwapo rufaa yake itatupwa.

No comments