AL AHLY YABANWA TOTAL CAF CHAMPIONS, ESPERANCE YAPETA

MABINGWA mara nane Ligi ya Mabingwa Afrika “Total CAF Champions League”, Al Ahly ya Misri licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini, lakini walibanwa kwa karibu muda wote wa mchezo.

Wits maarufu kama “Clever Boys”, walionyesha mchezo mzuri wa kushambulia muda wote wa mchezo kabla ya Ahmed Hegazi kuwafungia wenyeji bao hilo pekee.

Wengi wanaamini kwamba Al Ahly hawatafurukuta katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wikiendi hii mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Ukiachana na mechi hiyo na ile ya Yanga na Zanaco, miamba wa Tunisia, Esperance waliichapa timu ya Horoya kutoka Guinea kwa mabao 3-1, mchezo uliopigwa mjini Tades.

Nao miamba wa Morocco, Wydad Casadlanca waliichapa FC Mounana ya Gabon kwa bao 1-0, mfungaji akiwa William Jebor.


Aidha, wawakilishi wa Algeria, timu ya USM Alger iliichapa Rail Club Kadiogo ya Burkina Faso kwa mabao 2-0, mabao yote yakifungwa kipindi cha pili na Oussam Darfalou na Amir Sayoud.

No comments