Habari

ALEXIS SANCHEZ AIPA MKONO WA KWAHERI ARSENAL

on

Alexis Sanchez anataka kuachana na Arsenal mwishoni mwa msimu huu baada ya kukerwa na kocha Arsene Wenger aliyemsugulisha benchi kwenye mchezo muhimu dhidi ya Liverpool Jumamosi.

Katika mchezo huo ambao Arsenal ilikubali kichapoo cha bao 3-1, Sanchez aliingizwa kipindi cha pili.
Uhusiano wa Wenger na nyota huyo wa kimataifa wa Chile uliharibika zaidi katika mchezo wa kipigo cha bao 5-1 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya  Bayern Munich.

Vyanzo vya habari vinasema  katika mchezo huo Sanchez aliwashutumu wachezaji wenzake na aliendelea kufanya hivyo hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, hatua ambayo haikumfurahisha Wenger. 

Wachezaji wenzake wamebaini kuwa Sanchez amekuwa mtata sana katika wiki za hivi karibuni huku Wenger na maafisa wa klabu wakionyesha wazi kutovutiwa na tabia za mshambuliaji huyo mazoezini tangu kumalizika kwa mchezo dhidi ya Bayern.

Sanchez mwenye umri wa miaka 28 alishutumiwa na wachezaji wenzake wenye hasira baada ‘kususa’ katikati ya mazoezi wiki iliyopita sababu inayoaminika kuwa ilichangia Wenger kumweka benchi kwenye mchezo dhid ya Liverpool uliochezwa Anfield.

Ukweli kuwa Sanchez alionekana kufurahi wakati Liverpool wakipata bao la kwanza, unachochea habari za nyota huyo kuachana na Arsenal.

Paris Saint-Germain na  Juventus  zoet zipo tayari kumnasa Sanchez anayelipwa pauni 180,000 kwa wiki na inaaminika PSG wapo tayari kumpa pauni 300,000 kwa wiki.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *