Habari

ANDREA BELOTTI WA TORINO HAJUI PA KWENDA KATI YA MAN UNITED NA CHELSEA

on

 MSHAMBULIAJI
nyota wa klabu ya Torino, Andrea Belotti amesema kwamba ni kweli kuna klabu
kubwa zinamtaka lakini hajui aende wapi.
Belotti ambaye
amek,uwa mpachika mabao mahiri katika klabu hiyo, amesema kwamba anajua
anatakiwa na klabu mbalimbali lakini sio wakati wake sasa kutangaza kwamba
anakwenda wapi.
“Wakati
mwingine natakiwa kuulizwa kwamba nitabaki hapa kwa miaka mingapi kwa maana ya
kuongeza mkataba, sio kuniuliza tu kwamba nitakwenda wapi,” amesema.
Wakati nyota huyo anafunga magoli matatu “hat-trick” katika ushindi wa 3-1 ambao Torino waliupata Jumapili iliyopita dhidi ya Palermo katika Ligi Kuu ya Italia serie A, baadhi ya waandishi walitaka kujua kwamba baada ya hapo anakwenda wapi. 
 
Chelsea chini ya kocho Antonio Conte, Manchester United, Arsenal, FC Bayern Munich na Borussian Dortmund ni baadhi ya timu kubwa za Ulaya ambazo zinapendezwa na mshambuliaji huyo kijana aliyefunga magoli 21 msimu huu katika serie A.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *