ANDREA PIRLO AFICHUA SIRI ZA PEP GUARDIOLA

KUNA jamaa mmoja alikuwa anajua kufumania nyavu akiwa katika eneo lolote. Anaweza kuamua kucheza kama beki au kiungo na akakufunga, akija kushambulia anakuwa balaa zaidi.

Huyu anaitwa Andrea Pirlo na timu zote kubwa zilitamani kumsajili lakini wakashindwa. Wakati mwingine msimamo wake ukawa tofauti na matakwa ya wale wanaomtaka.

Juzi mkongwe huyo amesema kwamba anamshangaa sana kocha wa sasa wa Manchester City, Pep Guardiola akisema kwamba wakati mwingine hajui mtu wa kumsajili na kwa wakati gani.

Alisema kuwa, wakati kocha huyo alipokuwa anafundisha timu ya FC Barcelona ya Hispania alijaribu kumsajili lakini akamwambia kwamba haoni sababu.

“Wakati ule nilikuwa AC Milan na Pep kila mara alikuwa ananipigia simu niende lakini nikamwambia kuwa hana sababu ya kunisajili mimi,” alisema.

Pirlo amesema kwamba Guardiola alimwita katika ofisi yake pale Nou camp wakati AC Milan wanafanya mazoezi yao nchini Hispania kwa ajili ya kujiandaa kwa Ligi lakini alimkatalia na kumwambia kuwa haoni nafasi yake.

“Wakati ule ilikuwa mwaka 2010. Kwanza nilimwambia kabisa kwamba si rahisi kwa miamba hao wa San Siro kuniachia, lakini pia nikamwambia kwamba mbona ana wachezaji wa maana zaidi yangu,” alisema.

No comments