ANTONIO CONTE ASEMA CHELSEA BADO INA KAZI KUBWA KUJIHAKIKISHIA UBINGWA MSIMU HUU

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesisitiza kuwa bado wako katika mapambano makali ya kuwania pointi 21 ili waweze kutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.


Baada ya kushinda mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Stoke City kwa mabao 2-1, ilikuwa inaongoza Ligi ikiwa na pointi 13, lakini kocha huyo amedai kazi bado kubwa kuhakikisha timu yake inakuwa bingwa msimu huu.

No comments