ARGENTINA, BRAZIL WAENDELEA KUTAWALA SOKA DUNIANI

MATAIFA mawili ya Argentina na Brazil ni kama watawala wa soka la dunia hii.

Katika viwango vipya vya ubora duniani vinavyotolewa na Shirikisho la soka Duniani (FIFA), kila mwezi kwa sasa vinaonyesha baadhi ya mataifa kupanda katika nafasi.

Kwa upande wa orodha ya jumla Argentina bado wameendelea kuwa vinara wakifuatiwa na Brazil katika nafasi ya pili, huku mabingwa wa dunia, Wajerumani wakiwa nafasi ya tatu.

Kwa upande wa Afrika; Uganda bado wanaendelea kuongoza kwa Afrika Mashariki wakiwa nafasi ya 16 Afrika na 74 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 21 Afrika na 88 duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 24 Afrika na 93 duniani na Burundi nafasi ya 41 Afrika na 139 duniani.

Misri wao wameendelea kuwa vinara kwa kukwea nafasi mbili zaidi hadi nafasi ya 20, wakifuatiwa na Senegal walio nafasi ya 28, huku mabingwa wa michuano ya Mataifa, Cameroon nao wakikwea nafasi moja mpaka nafasi ya 32 duniani.


Mabingwa wa America Kusini, Chile wapo nafasi ya nne na Ubelgiji ndio wanakamilisha tano bora kwenye orodha hizo. Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika viwango kwa kuwa nafasi ya 158.

No comments